Breaking News

VIDEO: ZAIDI YA WATU 50 WAPOTEZA MAISHA KATIKA MAPOROMOKO YA ARDHI

Idadi ya watu waliofariki katika mkasa wa maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa inayonyesha katika eneo la Pokot Magharibi nchini Kenya imepanda na kufikia watu 52, amesema afisa wa serikali katika eneo hilo.
Idadi ya miili ambayo haijapatikana ni 22, baada ya mkasa huo kuyakumba maeneo ya Parua, Nyarkulian and Muino, kwa mujibu wa Gavana wa jimbo hilo, Profesa John Lonyangapuo.
Juhudi za kuipata na kuivuta miili kutoka kwenye matope zimekwmaishwa na usafiri baada ya barabara zinazokwenda katika maeneo hayo kuharibika.
Amesema kuwa nyumba 22,000 zimeharibiwa na maporomoko ya ardhi na kati ya watu 80,000 na 120,000 wamesambaratika au kuathiriwa na mafuriko hayo.
Waziri wa mambo ya ndani nchini Kenya Fred Matiang’i katika ujumbe wake wa Twitter ameeleza kuwa amelazimika kutua kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Eldoret alipokuwa akielekea katika maeneo ya mkasa wa maporomoko ya ardhi kutokana na hali mbaya ya hewa alipokuw aakijaribu kuelekea huko kuangalia shughuli za uokoaji:
Maafisa wanasema kuwa barabara zinazounganisha vijiji zimeharibika kutokana na mafuriko katika barabara na takriban daraja moja limeripotiwa kusombwa na maji.
Bwana Lonyangapuo. ametoa wito wa drarura kwa waziri wa mambo ya ndani nchini humo Fred Matiang’i akimuomba usaidizi wa helikopta kwa ajili za uokoaji katika maeneo yaliyoathiriwa na maporomoko ya ardhi.
Siku ya Jumamosi rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, alituma salamu za rambi rambi kwa familia zilizoathiriwa na mkasa huo.
”Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mkasa huu, kwa wale waliojeruhiwa na ambao wanaenelea kupokea matibabu katika hospitali mbali mbali, nawaombea uponyaji wa haraka” alisema rais Kenyatta.
Rais aidha aaliagiza ndege ya kijeshi kupelekwa katika eneo hilo kusaidia katika shughuli ya uokozi na kutoa wito kwa mamlaka katika eneo hilo kushirikiana na asasi za usalama kufanikisha oparesheni ya uokozi.
Chifu wa Nyarkulia Joel Bulal, amenukuliw na vyombo vya habari akisema kuwa kuwa shughuli za uokozi zinaenedelea huku na kuwatafuta wale ambao hawajulikani waliko.
Maporomoko hayo yalioathiri zaidi vijiji vya Nyarkulian na Parua,Haki miliki ya pichaMARK MEUT
Image captionJuhudi za kuipata na kuivuta miili kutoka kwenye matope zimekwmaishwa na usafiri baada ya barabara zinazokwenda katika maeneo hayo kuharibika
Kamishena wa jimbo hilo Apollo Okelo amesema watu wengine wengi huenda wamekwama chini ya matope na kuongeza kuwa shughuli ya kuwaokoa zinaathiriwana hali mbaya ya hewa.Kumeshuhudiwa mvua nyingi katika eneo la Afrika Mashariki na upembe wa Afrika kwa wiki kadhaa sasa.
Kijiji kizima kimesombwa na maji nchi Sudan Kusini huku visa ajaliya maporomoko ya ardhi ikiripotiwa Tanzania, Ethiopia na Somalia.
Wanasayansi wanasema hali mbaya ya hewa inatarajiwa kukumba baadhi ya nchi katika kanda hiyo kwasababu viwango vya joto katika bahari Hindi vinatarajiwa kupanda kupita kiasi cha kawaida, hali ambayo huenda ikasababisha mvua kubwa.



UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE