Breaking News

MILIONI 50 ZAWEKWA MEZANI SIMBA SC VS YANGA SC


Mchezo wa kwanza wa watani wa jadi kati ya Simba SC dhidi ya Yanga SC utapigwa January 04 2020 kwenye uwanja wa Taifa.

Kampuni ya GSM ambayo imekuwa ikitoa Milioni 10 kwa kila mchezo wa ligi ambao Yanga inashinda, imeahidi kutoka kitita cha Tsh Milioni 50 kwenye mchezo huo.

Afisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema GSM imetoa ahadi hiyo wakati anamkabidhi Sh 10 milioni Nahodha msaidizi Juma Abdul jana baada ya ushindi wa bao 3-2 dhidi ya JKT Tanzania.

"Katika mchezo wetu dhidi ya Simba wadhamini wetu GSM wanatatoa Sh 50 milioni hii ni kubwa kuliko, kwahiyo wachezaji hilo mkae mkijua kabisa tunahitaji ushindi katika mchezo huo," alisema


Aidha Nugaz amesema utaratibu huo utaendelea kwa michezo mingine huku ukubwa wa dau ukitegemea umuhimu wa mchezo.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE