Breaking News

MOURINHO ATOA AHADI HII SPURS

KOCHA mpya wa Tottenham, Jose Mourinho anasema kuwa katika klabu yake mpya ya Spurs kamwe hatafanya makosa aliyoyafanya
huko nyuma katika majukumu yake ya ukocha.

Mreno huyo amechukua nafasi ya Mauricio Pochettin Jumatano, akihitimisha miezi 11 ya kutofanya kazi ya ukocha tangu alipotimuliwa
Manchester United. Mourinho alijielezea kama mtu mnyenyekevu katika mkutano wake wa kwanza kama kocha wa Spurs, akisema
alitumia muda wake nje ya soka akielezea taaluma yake.

“Niligundua kuwa nilifanya makosa,”alisema.
“Sitafanya tena makosa yale yale. Sasa nitafanya makosa mapya, lakini si yale yale.” Mourinho, ambaye hata hivyo, hakuweka bayana
makosa anayoyazungumzia, aliongeza: “Mimi ni mnyenyekevu katika kazi yangu, na sio kwa mwaka jana ila kwa kila kitu, kuhusu
mabadiliko, matatizo na ufumbuzi. Simlaumu mtu yeyote.


“Ni jambo kubwa. Nilikwenda mbali zaidi…, “alisema kocha huyo mwenye maneno mengi.
Mourinho kipindi chake akiwa Manchester United kilimalizika Desemba mwaka jana baada ya timu hiyo kuwa pointi tisa nyuma ya vinara
wa Ligi Kuu, Liverpool. Pia aliripoti kufeli katika usajili wake wa Paul Pogba ambao uligharimu kiasi cha pauni milioni 89, ambao
ulikosolewa na mashabiki.

Kocha huyo wa zamani wa Porto, Chelsea na Real Madrid aliondoka Old Trafford akiendeleza tabia yake ya kutomaliza misimu minne mfululizo katika klabu moja.

“Nisiposhinda kamwe siwezi kuwa na furaha na hilo siwezi kulibadili,” aliongeza Mourinho.

“Hiyo ndio alama yangu. “Natumaini naweza kuwashawishi wachezaji wangu, kwa sababu ikiwa unafurahia kushindwa mechi ya soka ni
vigumu sana kuwa mshindi.

“Wakati fulani unatakiwa kufanya kazi na watu, ambao huwapendi na kufanya kazi vizuri. Huo ndio utaratibu
wetu na sifikiri kama naweza kuubadili.”

WACHEZAJI WAPYA
Mourinho alitumia kiasi cha pauni milioni 400 kwa kununua wachezaji wapya 11 wakati wa miaka yake miwili pale Manchester United,
lakini anaamini tayari ana wachezaji wazuri hapo Spurs.

“Zawadi kubwa niliyokuwa nayo mimi, sihitaji wachezaji wapya,”aliongeza.
“Kwa kweli nina furaha na hawa nilionao hapa. “Kikubwa nahitaji muda zaidi wa kuwa na wachezaji hawa. Nawajua kutokana na kucheza
dhidi yao, lakini huwezi kuwajua vizuri sana.”

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 ameanza kuifundisha timu hiyo ya Spurs ambayo iko katika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa imeshinda mechi tatu tu msimu mzima hadi sasa.

Hata hivyo, Mourinho, ambaye ameshinda mataji katika kila klabu aliyoifundisha, ana uhakika bahati ya klabu hiyo itarejea baada ya yeye
kutua hapo.

Alisema: “Hatuwezi kutwaa taji la Ligi Kuu msimu huu, lakini tunaweza kushinda msimu ujao…” Licha ya Tottenham kuanza vibaya
msimu, kuondoka kwa Pochettino Jumanne kulitokea kama kwa mshangao kwa wengi baada ya klabu hiyo kucheza fainali ya Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya msimu uliopita na kufungwa na Livepool.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE