RWANDA YAWAPOKEA WAHAMIAJI 117 WALIYOZUILIWA LIBYA
Wahamiaji 117 waliokuwa wamezuiliwa Libya wamewasili nchini Rwanda mapema leo asubuhi, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHR.
Wengi wa wahamiaji wa kundi hili la sasa wanatoka katika nchi za Eritrea na Somalia.
Muungano wa Ulaya awali uliilipa mamilioni ya euro kwa nchi ya Niger ambayo inawahifadhi wakimbizi zaidi ya 4,000 ambao walikuwa wanashikiliwa nchini Libya ili kuwazuwia kuendelea kuingia Ulaya.
Maafisa wa Rwanda wamesema kuwa hawana makubaliano na Muungano wa Ulaya, wala hawana faida rasmi kutokana na kuwapokea wakimbizi.
Kundi hili linafuatia Kundi jingine la wahamiaji 66 lililojumuisha na watu walio hatarini zaidi pamoja na watoto walio peke yao ambalo liliwasili nchini humo wakiwemo watoto.
Kikundi kilichowasili awali kiliwajumuisha miongoni mwa watu hao ambao baadhi yao walitoka mataifa ya upembe wa Afrika.
Kwa mujibu wa wizara ya masuala ya dharura nchini Rwanda wakimbizi hao pia watapewa hifadhi katika kituo cha wahamiaji cha Gashora ambacho tayari kinawahifadhi wakimbizi na wahamiaji 189 walioletwa Rwanda tarehe 26 Septemba na tarehe 10 Octoba 2019:
Wahamiaji hawa wataishi katika kituo cha muda kilichopo umbali wa saa moja kwa gari kutoka mjini Kigali.
Rwanda ilikubali kuwahifadhi wahamiaji 500 kwa ushirikiano na UNHCR, na Muungano wa Afrika ulitoa hakikisho la usafiri wao wa kutoka Libya kuelekea Rwanda, ili kuwaepusha na hatari ya kushambuliwa kwa roketi na kubakwa.
Haijafahamika wazi ni kwa muda gani wahamiaji hao watakuwa Rwanda na wana uhuru kwa kiwango gani kuondoka nchini humo
“Wakimbizi watakaotaka kuishi Rwanda daima watapewa ukimbizi ,” alisema Olivier Kayumba, katibu wa kudumu katika wizara ya udhibiti wa masuala ya dharura na masuala ya wakimbizi .
Zaidi ya wahamiaji 4,500 wanashikiliwa katika mahabusu baada ya ndoto yao ya kuvuka bahari ya Mediterranea kuelekea ulaya kukatizwa.
Maafisa wanasema miongoni mwa wahamiaji hao 66 ni wanawake na watoto walio katika hali mbaya kiafya na vyombo vya habari vilidhibtiwa kuwaona.
Hatua ya kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda ilichukuliwa baada ya juhusi za ufadhili mbali mbali za kudhibiti wimbi la wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya kupitia safari hatari ya bahari ya Mediterranean kugonga mwamba.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji linasema kuwa zaidi ya watu 45,500 waliingia Ulaya kupitia bahari ,kiwango hicho kikiwa kimepungua kwa 30% ikilinganishwa na mwaka 2018.
Kituo kikubwa cha kuwaokoa wahamiaji kinachoendeshwa na Umoja wa Mataifa kipo katika taifa la Niger ambako kuna njia ya wahamiaji ya kaskazini mwa Afrika kwa sasa kimefurika wakimbizi sawa na kile cha Umoja huo kilichopo katika mji mkuu wa Libya Tripoli ambacho kina jumla ya wahamiaji na wakimbizi 1,000.
Mataifa ya ulaya yamekuwa yakiwashughulikia kwa njia isiyofaa wahamiaji katika juhudi za kudhibiti wimbi la wakimbizi , na wamekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa badhi ya mashirika ya haki za binadamu ambayo pia yaliwalaumu kwa kukubali kukubali idadi ndogo ya wahamiaji.Wahamiaji wa Libya wakiwa safarini kuelekea nchini Rwanda
Ni kundi dogo tu la watu 2,900 ambao waliokolewa katika kituo cha Niger waliopata uhamiaji katika mataifa ya Ulaya na kwingineko.
Takriban wahamiaji 6,000 kutoka mataifa ya Eritrea, Ethiopia, Somalia, Sudan na mataifa mengine bado wako katika vizuizi vinavyoendeshwa na wanamgambo wa Libya wanaoshutumiwa kuwatesa. Baadhi ya wahamiaji wamekuwa wakizuiwa katika bahari ya Mediterranean na walinzi wa mwambao wa Libya wanaodhaminiwa na Muungano wa Ulaya, ambao wamekuwa wakilengwa na shutuma za mateso dhidi ya wahamiaji.
Wengi miongoni mwa wahamiaji wanatoka katika mataifa ya upembe wa Afrika yakiwemo mataifa ya Somalia, Eritrea na Ethiopia.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE