Breaking News

SIMBA YATOA WAWILI TUZO ZA MCHEZAJI BORA WA MICHUANO YA VILABU AFRIKA


Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere pamoja na aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo msimu uliopita Emmanuel Okwi ni miongoni mwa wachezaji 20 waliotajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya vilabu barani Afrika kwa mwaka 2019.

Okwi na Kagere walikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichofika hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu wa 2018/19 lakini kwa sasa Emmanuel Okwi ameondoka klabuni hapo na kutimkia Al Itihad ya Misri.

Katika msimu huo, Meddie Kagere raia wa Rwanda aliifungia Simba mabao sita huku Emmanuel Okwi raia wa Uganda akifunga mabao manne kwenye michuano hiyo.

Sherehe za tuzo hizo zitafanyika Januari 7, 2020 nchini Misri.

ORODHA KAMILI YA WAPINZANI WA OKWI NA KAGERE, HII HAPA

1. Ali Maaloul - Tunisia & Al Ahly.
2. Anice Badri - Tunisia & Esperance.
3. Denis Onyango - Uganda & Mamelodi Sundowns.
4. Emmanuel Okwi - Uganda & Simba.
5. Ferjani Sassi - Tunisia & Zamalek.
6. Fousseny Coulibaly - Cote d'Ivoire & Esperance.
7. Franck Kom - Cameroon & Esperance.
8. Herenilson - Angola & Petro de Luanda.
9. Ismail El Haddad - Morocco & Wydad Casablanca.
10. Jean Marc Makusu - DR Congo & AS VITA.
11. Kodjo Fo Doh Laba - Togo & RS Berkane / Al Ain.
12. Mahmoud Alaa - Egypt & Zamalek.
13. Meddie Kagere - Rwanda & Simba.
14. Meschack Elia - DR Congo & TP Mazembe.
15. Taha Yassine Khenissi - Tunisia & Esperance.
16. Tarek Hamed - Egypt & Zamalek.
17. Themba Zwane - South Africa & Mamelodi Sundowns.
18. Trésor Mputu - DR Congo & TP Mazembe.
19. Walid El Karti - Morocco & Wydad Casablanca.
20. Youcef Belaïli - Algeria & Esperance / Ahli Jeddah.

UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE