Breaking News

MASAU BWIRE AMJIBU MANARA ISHU YA KUPEWA IPHONE

Heshima yangu, kama nilivyoumbwa si ya kujivuna, ni kuheshimu kila mtu na hali yake, masikini au tajiri, ndivyo nilivyoumbwa.

Kudamshi mie sikusubiri niwe msemaji, nitakuwa mpuuzi nikianza kutangaza kwa umma kwamba, navaa vizuri naenda kujirusha, kwa mwenye akili, mwenye familia, anayeijali hawezi kutamba kwa hilo.

Simu ni kitu gani, mawasiliano tu brother, simu zangu ni ndogo kiumbo lkn ni kubwa kiuwezo, na ukiona mtu anajitapa kwamba anachokitu fulani ambacho fulani hana, mchunguze vizuri, hayuko sawa huyo. Mimi siyo limbukeni, niko vizuri.

Uswekeni sitaki hata kulizungumzia, lakini maisha yangu yako poa, naitunza familia, inaishi vizuri, hatuna shida kwa kweli.

Sijui kujirusha, ili iweje?
Tangu nizaliwe sijawahi kuonja harufu ya pombe, wala kwenda disco, hata soda sinywi, na huo ushatani mwingine kwangu mwiko kabisa, naishi maisha ya kumfurahisha Mungu pamoja na wanadamu wenye akili tu...

Mimi nazungumzia mpira, sikuajiriwa Ruvu Shooting kuzungumzia watu na maisha yao, wala kujivuna kwamba nina hiki, ambacho fulani hana!

Nisameheni katika majibizano ya kutafuta kuonekana mimi ni bora kuliko wengine, ninavyo wasivyonavyo, siyo tabia yangu.

Karibuni Mabatini, tufurahi pamoja.

Mungu wetu ni mwema.

Na Masau Bwire, Msemaji wa Ruvu Shooting
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE