TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMANNE NOVEMBER 26,2019
Mshambuliaji wa England Raheem Sterling, mwenye umri wa miaka 24, anasubiri kuona ikiwa meneja wa Manchester City Pep Guardiola atajitolea kuiboresha klabu hiyo kabla ya kusaini mkataba mpya . (FourFourTwo)
Mshambuliaji wa England Raheem Sterling, anasubiri kuona ikiwa meneja wa Manchester City Pep Guardiola ataboresha timu hiyo
Pep amezionya klabu zenye nia ya kumchukua, Mikel Arteta ambaye ametokea kupigiwa upatu kuchukua nafasi ya ukocha pale Arsenal na Everton, Guardiola amesisitiza Arteta ataendelea kubakia City. (Times)
Meneja wa Tottenham, Jose Mourinho amemuomba wakala Jorge Mendes kuendelea kumpa taarifa kuhusu wachezaji Ruben Dias mlinzi katika klabu ya Benfica ya Ureno mwenye umri wa miaka , 22, pamoja na kiungo wa kati Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 25, wa klabu ya Sporting Lisbon. (90min)
West Ham wanaangalia uwezekano wa kumchukua meneja wa Sheffield United Chris Wilder kama meneja wao ajaye, ikiwa wataamua kumfuta kazi meneja wao sasa Manuel Pellegrini. (Mirror)
Pellegrini tayari ameonywa kwamba matokeo ya timu lazima yawe bora wakati wa mazungumzo na bodi ya the Hammers. (Times)
Meneja wa Everton Marco Silva anaweza kupewa fursa ya kuongoza gemu mbili zaidi iwapo mhisani wakuu Farhad Moshiri na mwenyekiti wa klabu hiyo Bill Kenwright watakuwa wakijadili juu ya meneja mbadala. (Mail)
Kocha wa zamani wa Toffees Sam Allardyce anasema ni wazi wachezaji hawachezi tena kwa ajili ya Silva. (Talksport)
Mkurugenzi wa soka wa klabu ya Everton Marcel Brands na meneja Silva wamefanya mazungumzo juu ya mkakati wa kumrejesha katika klabu hiyo mlinda mlango mreno Joao Virginia kutoka Reading anakocheza kwa mkopo(echo)
The Foxes walilazimika kumzuia mlinzi kutoka Croasia mwenye umri wa miaka 22 Filip Benkovic kwenda Stoke City kwa mkopo katika msimu uliopita baada ya kushindwa kusaini mkataba na Harry Maguire ambaye alitarajiwa kuziba pengo lake. (Athletic, via Leicester Mercury)Everton itafanya mazungumzo na mlindalango Mreno Joao Virginia anaechezea Reading
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema “anampenda” mshambuliaji Mfaransa Kylian Mbappe, mwenye umri wa miaka 20, huku klabu yakeikijiandaa kuwapokea Paris Saint-Germain katika Ligi ya mabingwa. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Chelsea mfaransa N’Golo Kante anasema uamuzi wake wa kutohamia katika klabu ya Ufaransa PSG ulikuwa ni “wa kimchezo” (Canal Plus, via Mirror)
Rais wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis ameitoza faini ya zaidi ya pauni milioni 2.1 kwa timu ya kwanza kufuatia “uasi ndani ya klabu “. (ESPN)
Mlinzi wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti, mwenye umri wa miaka 26, amesema haiwezekani kurudi Lyon huku, klabu ya Arsenal ikimtaka. (Sport)
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE