TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATANO NOVEMBER 27,2019
Meneja wa Wolves Nuno Espirito Santo ndiye meneja aliye mstari wa mbele kuchukua nafasi ya Unai Emery kama meneja wa Arsenal (Mail)
Wahudumu wa Arsenal wanaamini kuwa kocha Unai Emery atafutwa kazi, lakini bado anatarajiwa kuongoza timu katika mechi ya Ligi ya europa dhidi ya Eintracht Frankfurt. (Goal)
Barcelona na Real Madrid wako tayari kumhamisha mshambuliaji wa Arsenal Mgabon Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Arsenal mwenye umri wa miaka 30 (Mirror)
Timu ya Ligi kuu ya Uhispania Barcelona wanaongoza juhudi za kumpata Aubameyang. (Star)
Manchester United wanaamini watabakia kuwa mstari wa mbele katika kusaini mktaba na kiungo wa mashambulizi wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 19 kutoka England Jadon Sancho mwaka ujao.(Telegraph)
Wakati huo huo, Everton inakabiliwa na ushindani kutoka West Ham wa kumchukua David Moyes kama kocha wao ajae. (Mirror)
Naibu mkurugenzi mkuu mtendaji wa United Ed Woodard anasema kulikuwa na ”tofauti” ya maoni juu ya mchezaji mmoja au wawili ” baina ya klabu na meneja wa zamani wa Jose Mourinho. (Mirror)
Mkataba mpya wa kiungo wa safu ya mashambulizi wa England Raheem katika Manchester City unaweza kumuwezesha kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 kusaini mkataba wa malipo zaidi ya pauni 350,000 kwa wili na Kevin de Bruyne. (Sky Sports)
Wakala wa winga wa Mancheter City Mjerumani Leroy Sane amekutana na klabu ya Bayern Munich, lakini machampioni hao wa Bundesliga watakiwa kusubiri hadi msinu ujao kusaini mkataba na kijana huo mwenye umri wa miaka 23. (Goal)
Manchester United, Tottenham na Liverpool ni miongoni mwa klabu zinazoshindania kusaini mkataba na mshambuliaji wa Peterborough United mwenye umri wa miaka 17 Muingereza Ricky-Jade Jones. (Mail)
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE