VIDEO: BREAKING: JAFO ATANGAZA MATOKEO UCHAGUZI S/MITAA
WAZIRI Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, ametangaza matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda vijiji 12,260 sawa na asilimia 99.9, pia kimeshinda katika mitaa 4,263 sawa na asilimia 100, huku kikishinda vitongoji 63,970 sawa na asilimia 99.4.
“Kwa upande wa Chadema, wenyeviti wa vijiji imeshinda nafasi moja, haikufanikiwa kupata mtaa, lakini wenyeviti wa vitongoji imepata nafasi 19, wajumbe kundi la wanawake imepata nafasi 39 na wajumbe kundi mchanganyiko imepata nafasi 71.
“Chama cha CUF nafasi ya vijiji wamepata nafasi moja, wamepata mitaa miwili, wajumbe kundi la wanawake wamepata nafasi tatu, na wajumbe kundi mchanganyiko wamepata nafasi 14.
“Chama cha ACT Wazalendo, hakikufanikiwa kupata mwenyekiti wa kijiji, hakikufanikiwa kupata mtaa, lakini kimefanikiwa kupata mwenyekiti wa kitongoji mmoja, wajumbe kundi la wanawake wamepata nafasi moja, na wajumbe kundi mchanganyiko wamepata nafasi 11,” amesema.