Breaking News

Video: Fahamu upekee wa boti ya kisasa ya Kilimanjaro VII ya Bakhresa

Boti mpya ya Kilimanjaro VII inayomilikiwa na Bakhresa Group chini ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu imewasili leo Zanzibar kutoka kiwandani Australia.

Boti hiyo itakayokuwa na huduma za kisasa zaidi hapa Tanzania, imefika Zanzibar ikiwa imebebwa juu ya meli maalum.
Kwa mujibu wa kampuni ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries, boti hiyo inafanyiwa ukaguzi na kukamilisha taratibu nyingine za kimamlaka kabla ya kutangazwa muda wa kuanza huduma zake.

UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE