Breaking News

VIDEO YA WIMBO WA HARMONIZE 'UNO' YAREJESHWA YOUTUBE KWA KISHINDO

MTAYARISHAJI wa muziki kutoka nchini Kenya, Magix Enga ameomba msamaha kwa msanii wa Bongo Fleva, Harmonize kufuatia kui-block ngoma yake ya UNO kwa madai kwamba ameiba biti ya wimbo uitwao DUNDAING.

Siku chache zilizopita Magix aliwasilisha malalamiko yake kwenye mtandao wa YouTube juu ya Beat ya wimbo wa Harmonize, UNO kufanana na mdundo wa wimbo wa DUNDAING aliyouandaa yeye na kuimbwa na msanii King Kaka.

Baada ya kikao cha muda mrefu na mawakala wa YouTube Afrika Mashariki Ngoma Magix Enga ametangaza msamaha kwa Harmonize na kuirudisha YouTube video hiyo ya UNO.

Magix Enga ameandika; “With #CLEMO @Ngomma ✌️Growth of East African music is bigger than all of us. And for this reason i have decided that I will release my copyright strike on Uno by Harmonize. I have decided to forgive the guy🇹🇿 Nitarudisha Uno by Harmoize Pale YouTube Wakati wowote.”

Baadaye akaandika tena; “Everybody say Uno ✌🏾🇰🇪🇹🇿 Now available on YouTube both audio and video.

UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE