WATANZANIA 200 HUAMBUKIZWA VVU KILA SIKU
Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Leonard Makombo, amesema kuwa zaidi ya watanzania 200 huambukizwa virusi vya ukimwi VVU kila siku hivyo kufanya idadi ya maambukizi kuwa 72,000 kwa mwaka.
Amebainisha hayo juzi alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo mwaka huu yamepangwa kufanyika kitaifa jijini mwanza.
Amesema kuwa takwimu zinaonesha vijana wenye umri wa kati ya mika 14 na 24 ndiyo wanaongoza kwa maambukizo, wakichukua asilimia 40 ya maambukizo mapya.
Amesema ” Kwa kuzingatia kwamba takriban watu 200 wanaambukizwa VVU kila siku, 80 ni kutoka kundi hilo la vijana”
Katika maadhimisho hayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye viwanja vya Furahisha jiji Mwanza, ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali, upimaji wa hiari wa VVU na utoaji wa huduma za ushauri nasaha.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE