Breaking News

WASIWASI WATANDA KWA MABOSI WA ARSENAL, KISA UNAI

Klabu ya Arsenal yaingiwa na hofu juu ya baadhi ya nyota wake wakubwa huwenda wakalazimisha kuondoka kama endapo Kocha Mkuu wa timu hiyo, Unai Emery ataendelea kusalia hadi msimu ujao.
Arsenal fear their top stars will be forced to consider their futures if Unai Emery stays
Kwa mujibu wa Sportsmail, inadai kuwa Mkuu wa kitengo cha soka, Raul Sanllehi na Mkurugenzi wa Ufundi, Edu Gaspar wamefanya mazungumzo na Emery kuhusiana na swala hilo, baada ya sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya Southampton siku ya Jumamosi.
Wasiwasi umezidi kuongezeka kwa Emery, kama kocha huyo ataendelea kusalia Arsenal basi kunauwezekano mkubwa kuwapoteza wachezaji wao nyota ambao tayari wanaamini wangeweza kukaa hapo kwa muda mrefu kama kocha huyo ataondoka, na kama hatoondoka basi watakuwa na maisha mafupi sana the Gunners.
Emery is under huge pressure with his side already eight points adrift of the top four
Wachezaji wakubwa ndani ya kikosi hiko wanatilia shaka njia na mbinu za ufundishaji za Emery, wengi wakiamini kuwa huwenda zisizae matunda na hivyo kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Champions League msimu ujao.
Mabosi wa The Gunners wanaimani kuwa, kuendelea kutoridhishwa na mbinu za kocha huyo kutaweza kusababisha kwa wachezaji hao kuondoka Emirates.
Tayari mpaka sasa wachezaji muhimu kama Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette wapo kwenye mazungumzo ya kupatiwa mikataba mipya lakini wawili hao hadi sasa hakuna aliyeonyesha niya ya kuanguka saini.
Wote wanahitaji kushiriki kucheza michuano ya Champions League lakini kwa mwenendo wa klabu ya Arsenal unaonyesha wazi kuwa chini Emery wananafasi finyu sana ya kutimiza malengo hayo.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE