Breaking News

WAWILI WAPIGWA STOP KUSEPA YANGA

WASHAMBULIAJI wa Yanga Mganda, Juma Balinya na Mkongomani, David Molinga ‘Falcao’ wamehakikishiwa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ licha ya ubonge wao.

Wawili hao inakuwa ni kama wamepigwa STOP juu ya kuondoka kwao msimu huu wa dirisha dogo na badala yake wana asilimia kubwa ya kuendelea na majukumu ndani ya kikosi.

Awali, aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Mkongomani, Mwinyi Zahera aliwahi kutamka kuwa hatawatumia wachezaji hadi watakapopunguza uzito, hii nikufuatia kunenepa sana, lakini Mkwasa yeye amewatuliza kimtindo kwa kuwaahidi kuwapa nafasi ya kucheza.

Yanga chini ya Mkwasa tayari imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza wa Ligi Kuu Bara walioupata mara baada ya kuwafunga Ndanda FC bao 1-0 lililofungwa na Patrick Sibomana.

Mkwasa alisema kuwa hataangalia ukubwa wa mwili wa mchezaji yeyote, zaidi anaangalia kiwango pekee kitakachomfanya apate nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza mazoezini.

Mkwasa alisema wachezaji wote wa Yanga wana viwango vikubwa vya kucheza soka, kikubwa amemtaka kila mmoja kujituma na kutimiza majukumu yake ya ndani ya uwanja, hiyo ndiyo itakayompa nafasi katika kikosi cha kwanza.

Aliongeza kuwa, amewaona wachezaji wote katika mazoezi ya siku mbili aliyofanya na timu hiyo, mengi ameyabaini ikiwemo tatizo la kisaikolojia ambalo amepanga kulimaliza kwa haraka kwa kukaa na wachezaji wake ili kuhakikisha kila mmoja anatimiza majukumu yake ya uwanjani.

“Kwangu kila mchezaji ana nafasi ya kucheza bila ya kuangalia tatizo la ukubwa wa mwili ambalo kocha aliyepita alikuwa akilalamika kuwa wapo baadhi yao ni wanene, hawana nafasi ya kucheza katika timu yake.

“Mimi ninaangalia uwezo wa mchezaji siyo mwili, hata kama akiwa na mwili mkubwa lakini akiwa anafunga mabao uwanjani sioni sababu ya kutomtumia na ili mchezaji apate nafasi ya kucheza ni lazima anishawishi mazoezini.

“Hivyo, kwangu huyo Balinya na Molinga bado wana nafasi katika kikosi changu, ninaamini kadiri siku zinavyokwenda watakaa sawa na kuonyesha viwango vikubwa, kama unavyofahamu timu nimeikuta katikati hivyo ninahitaji muda wa kukaa nao zaidi,” alisema Mkwasa.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE