Breaking News

WAWILI WASEPA MAZIMA YANGA

Taarifa za kuaminikia kutoka ndani ya viunga vya Yanga imebainisha kuwa nyota Issa Bigirimana na Maybin Kalengo hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kuelekea usajili wa dirisha dogo.

Nyota hao walipewa ruhusa kurejea makwao wakikabiliwa na changamoto za majeruhi, huenda wasirudi tena. Imebainika kuwa Kalengo alitua Yanga kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Baada ya kupata majeraha ambayo yatamuweka nje kwa muda mrefu, Yanga italipia gharama za matibabu yake lakini inamrejesha katika klabu yake ya Zesco United.

Inaelezwa Bigirimana hakufikia makubaliano yaliyowekwa katika mkataba wake, Yanga imeona kuendelea kuwa nae ni hasara kwani muda mwingi amekuwa majeruhi.

Nyota mwingine ambaye amekalia kuti kavu ni beki Mustafa Suleyman ambaye kiwango chake bado hakiwashawishi mabosi wa Yanga.

Walinzi wazawa Ally Ally na Ally Mtoni wameonyesha kuwa na uwezo zaidi yake hivyo haitakuwa rahisi kwake kuendelea kubaki Yanga wakati hana uhakika wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza huku akiwa mchezaji wa kigeni.

Mustafa alipaswa kuwapa changamoto wachezaji wazawa lakini imekuwa tofauti, wachezaji wazawa wanampa changamoto yeye.

Ni dhahiri Yanga itakuwa na nafasi sio chini ya tatu, kuongeza nyota wa kigeni katika dirisha dogo, ambapo tetesi zimekuwa nyingi kuhusu nyota wa kigeni ambao wanatajwa kuwa watasajiliwa.

Kila kitu kitakuwa wazi katika kipindi cha wiki tatu pale dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa December 16.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE