Breaking News

HATUTAPUUZA TUHUMA ZA KABWILI: MANARA

Afisa Habari wa Klabu ya Simba SC, Haji Manara amesema kuwa leo klabu hiyo itatoa msimamo wake kuhusu tuhuma za rushwa zilizotolewa na mlinda lango wa Yanga Ramadhani Kabwili.

Manara amesema tuhuma hizo zina athari kubwa kwa Simba hivyo ni lazima wachukue hatua.

"Moja ya jukumu langu kuu Simba licha ya kuisemea hii klabu ,lakini nnao wajibu wa kuitangaza na kulinda taswira ya Taasisi hii," amesema Manara

"Narudia tena na tena ,hili alilozungumzia mchezaji huyu tukikubali tuliache au kulipuuza litaleta athari kubwa kwetu na kwa ustawi wa Soka letu nchini"

"Bila shaka yoyote Watanzania leo mtasikia msimamo wetu juu ya tuhuma chafu dhidi ya Machampioni wa taifa hili, yapo ya kupuuza ila sio hili"

Jana akiwa katika mahojiano na East Africa Radio, Kabwili alidai kuwa msimu uliopita kuna viongozi wa Simba walimuahidi kumnunulia gari aina ya IST kama atafanya makosa ili apewe kadi ya njano katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania.


Wakati huo Kabwili alikuwa na kadi mbili za njano ambapo baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania, mchezo ambao ulikuwa ukifuata ulikuwa wa watani wa jadi (Simba SC vs Yanga SC).

UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE