KABENDERA AENDELEA KUSOTA MAHABUSU
KESI ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera imeahirishwa baada ya Jamhuri kudai upelelezi bado haujakamilika
Wakili wa Serikali, Gloria Mwenda, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mchakato wa majadiliano baina ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na mtuhumiwa (Erick Kabendera) wa namna ya kuimaliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili bado unaendelea.
Wakili Mwenda ameieleza mahakama kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika na hivyo akaiomba mahakama kuipangia tarehe nyingine ya kuitaja kesi hiyo.
Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Mtega ameiahirisha kesi hiyo hadi Februari 10, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa. Katika kesi hiyo, Kabendera anawakilishwa na mawakili Reginal Martin na Fulgence Massawe.
Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Sh 173 milioni.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE