KMC YAWAPA WAJEDA DILI LA UJENZI WA UWANJA WAO
MANISPAA ya Kinondoni leo Jumatatu, Januari 27, 2020, imetiliana saini na Jeshi la Wananchi kikosi cha 361 KJ kilichopo Lugalo jijini Dar es Salaam kuanza rasmi ujenzi wa Uwanja wa mpira wa manispaa hiyo uliopo Mwenge Dar, pamoja na ujenzi wa jengo la Utawala litakalojengwa Makao Makuu ya Manispaa hiyo, Magomeni Dar.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari baada ya kutiliana saini Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta amesema mara nyingi wamekuwa wakiwatumia wanajeshi hao kwenye shughuli mbalimbali za ujenzi na hakuna siku ambayo waliwahi kuwaangusha hivyo anahamini hata kwenye mradi huo utakuwa na ubora wa kuridhisha na kukamilika kwa wakati.
Naye msimamizi wa ujenzi huo kutoka kikosi cha 361 KJ, Luteni Kanali, David Michael Luoga amesema ujenzi huo utaanza hivi karibuni kukamilika mapema iwezekanavyo na kuiomba manispaa hiyo kuwasilisha vifaa vya ujenzi huo kwa wakati.
HABARI:NEEMA ADRIAN | PICHA: RICHARD BUKOS
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE