KAULI YA SIMBACHAWENE BAADA YA KUAPISHWA KUWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI
Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene ameahidi kushirikiana na viongozi wengine kuleta matokeo chanya yanayotarajiwa na Watanzania
Simbachawene ameapishwa leo Jumatatu Januari 27, 2020 Ikulu, Dar es Salaam baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli kuongoza wizara hiyo akichukua nafasi ya Kangi Lugola ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Simbachawene amesema ataviheshimu vyombo vya usalama kufanya kazi yake huku yeye akishughulika na mambo ya utawala.
“Pale ambapo vyombo vinafanya makosa kazi yangu ni kukutaarifu kwamba kuna mambo hayapo sawa, lakini mimi sina cheo chochote na wala sina nyota yoyote na hukunipa nyota hapa lao.”
“Umenipa jukumu nikusaidie katika kusimamia vyombo hivi ambavyo kwa sehemu vinafanya kazi ya ulinzi na usalama na ninatambua mimi sio amiri jeshi mkuu,” amesema Simbachawene
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE