SADIO MANE NJE WIKI TATU
Inaelezwa kuwa mshambuliaji wa Liverpool na Senegal, Sadio Mane anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu kufuatia maumivu ya nyama za paja aliyoyapata kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers wiki iliyopita.
Msenegali huyu anaweza kurejea dimbani kwa muda mwafaka kabla Liverpool haijaikabili Atletico Madrid kwenye hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Februari 18.
Mane alikosekana katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Shrewsbury jana Jumapili. Bado Liverpool haijatoa taarifa kamili lakini inaelezwa kuwa atakosekana pia katika michezo dhidi ya West Ham na Southampton wiki hii.