Breaking News

KOCHA YANGA AFUNGUKA ISHU YONDANI KUTOONEKANA


Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema timu hiyo haiwezi kubembeleza mchezaji kwa kuwa anaamini hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu.

Eymael ametoa kauli hiyo kufuatia mkasa unaomkabili beki kisiki Kelvin Yondani ambaye amekosekana kwenye timu kwa takribani wiki mbili.

Mbelgiji huyo amesema Yondani alikosa mazoezi kwa takribani siku sita akitoa sababu kuwa anaumwa huku pia akishindwa kucheza mechi dhidi ya Azam Fc akitoa sababu ya kuumwa tumbo.

"Kelvin hakufanya mazoezi kwa siku sita, hata mchezo dhidi ya Azam alidai anaumwa tumbo na hakupatikana hata tulipokuwa tunaenda Singida hatukuweza kumpata hewani simu yake ilikuwa haipatikani"

"Tuliporudi naye akarejea na kusema amepona. Wachezaji wanapaswa kujua kuwa ni lazima twende katika uelekeo mmoja kama timu sichezeshi majina bali nachezesha timu, na hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya timu, yeyote ataondoka lakini Yanga itakuwepo," amesema Eymael


Yondani tayari amerejea kikosini akiendelea na mazoezi na wachezaji wengine hata hivyo jana Eymael alimuweka nje nafasi yake akimtumia Said Juma Makapu.

UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE