SIMBA KUJIBU TUHUMA ZA KIPA WA YANGA
Uongozi wa klabu ya Simba umesema kuwa utatoa tamko kujibu tuhuma zilizotolewa na mlinda lango wa Klabu ya Yanga Ramadhani Kabwili kuwa msimu uliopita kuna viongozi wa Simba walimuahidi kumuhonga gari aina ya IST ili apate kadi ya tatu ya njano na hivyo akose mchezo wa pili wa ligi kuu uliozihusisha Simba na Yanga.
Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema watazungumza na wanahabari kujibu tuhuma hizo lakini pia amemtaka Kabwili aandae ushahidi kwani watachukua hatua za kinidhamu kwani kitendo alichofanya kinaichafua Simba.
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeiagiza kamati ya Maadili kuanza uchunguzi wa tuhuma hizo
Aidha taarifa ya TFF imesema tayari imetoa taarifa kwa vyombo vya usalama ili kuchunguza tuhuma hizo.