PABLO MARI ATUA ARSENAL KUFANYA VIPIMO
BEKI Mhispania, Pablo Mari, alisafiri hadi London juzi Ijumaa kwa ajili ya kufanya vipimo Arsenal, kwa mujibu wa taarifa.
Picha moja ilionekana kwenye Twitter ikimuonyesha Mari akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Ufundi wa Arsenal, Edu kwenye Uwanja wa Ndege wa Galeao jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Kwa mujibu wa ESPN, beki huyo wa kati wa Flamengo, 26, anakaribia kukamilisha usajili wake Arsenal.
Arsenal wanahitaji beki wa kati baada ya kuumia kwa Calum Chambers na kuendelea kusuasua kwa David Luiz, Shkodran Mustafi na Sokratis Papastatho poulos.