'SERENGETI GIRLS' YAICHAPA BURUNDI NA KUSONGA MBELE KUFUZU KOMBE LA DUNIA U17 WANAWAKE
Timu ya taifa ya wasichana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 imefanikiwa kusonga mbele katika mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2020 nchini India baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Burundi bao pekee la Protasia Mbunda leo Uwanja wa Intwari mjini Bujumbura.
Tanzania 'Serengeti Girls' imefanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 6-1 baada ya kushinda 5-1 kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Jijini Dar es Salaam Januari 12 na sasa watamenyana na mshindi wa jumla kati ya Uganda na Ethiopia zitakazorudiana kesho.
Katika mchezo wa kwanza Uganda ilishinda 2-0 Januari 11 Jijini Kampala.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE