SIMBA YAICHAPA MWADUI NA KUTINGA 16 BORA (ASFC)
Klabu ya Simba SC imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo kwa Simba SC ni sawa na kulipa kisasi baada ya kuchapwa 1-0 na Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Jumatano ya Oktoba 30, mwaka jana katika Uwanja wa CCM Kambarage, Mjini Shinyanga bao pekee la Gerald Mathias Mdamu.
Na haukuwa ushindi mwepesi kwa Simba SC, kwani na leo walitanguliwa kwa mara nyingine Gerald Mathias Mdamu akiwatungua dakika ya 35 akimalizia krosi nzuri ya Venance Ludovic, aliyemtoka kiungo Mkenya, Francis Kahata Nyambura upande wa kulia.
Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandonbroeck ikafanikiwa kusawazisha katika dakika ya 45 na ushei kwa bao la kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama baada ya kuwatoka mabeki wa Mwadui FC kufuatia pasi ya kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Dilunga.
Kipindi cha pili timu zote zilirejea kwa tahadhari, zikishambulia kwa tahadhari na kujilinda zaidi, lakini zikiwa zimesalia dakika tano mchezo kumalizika, Francis Kahata akasahihisha makosa yake kwa kuifungia Simba SC bao la ushindi kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomari Salum Kapombe.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE