SIMBA YATOA UFAFANUZI ISHU YA ITC YA KICHUYA NA MIQUISSONE
Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha kuwa nyota wake wapya Shiza Kichuya na Luis Miquissone hawatakuwa sehemu ya kikosi kwa kuwa vibali vyao (ITC) bado havijawasili.
Taarifa iliyotolewa na Simba mapema leo imebainisha kuwa tayari klabu imewasilisha maombi kwa shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kuomba kupatiwa kibaki cha muda ili kumtumia Miquissone.
Aidha kwa upande wa Kichuya, bado klabu ya Pharco Fc ya Misri haijajibu maombi yaliyopelekwa na uongozi wa Simba kuomba kibali chake.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE