THOMAS ULIMWENGU AREJEA TP MAZEMBE
Klabu ya TP Mazembe kupitia page yake ya Instagram imetangaza kurejea kwa mchezaji wake wa zamani mtanzania Thomas Ulimwengu.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Ulimwengu amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia miamba hiyo ya soka Afrika.
Ulimwengu aliondoka Mazembe mwaka 2016 akiwa na ndoto ya kwenda kucheza soka Ulaya lakini kwa bahati mbaya haikuwa kama watu wengi walivyotamani baada ya nyota huyo kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.
Katikati ya mwaka 2017 na 2018 alijaribu bahati yake katika vilabu viwili vya Ulaya, Eskilstuna (Sweden) na FC Sloboda Gorazde (Bosnia) huku akiwa na imani huenda ikiwa mwanzo wa safari yake ya kupata vilabu vingine vikubwa vya Ulaya.
Baadae Ulimwengu alirejea tena Afrika na kujiunga na Al Hilal ya Sudan lakini hakudumu kwa muda mrefu akajiunga na JS Soura ya nchini Algeria.
Na kesho Jumatano ya January 29 Ulimwengu atatambulishwa rasmi na klabu hiyo Mjini Lubumbashi DR Congo.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE