Breaking News

YANGA YAMUUNGA MKONO KABWILI ISHU YA HONGO KUTOKA SIMBA


Uongozi wa Klabu ya Yanga SC, umesema uko pamoja na mlinda lango wake Ramadhani Kabwili ambaye jana alifichua tukio la jaribio la hongo alilofanyiwa na baadhi ya viongozi wa klabu ya Simba msimu uliopita.

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema pamoja na kuwa wachezaji hawaruhusiwi kungea na vyombo vya habari, lakini kwa kuwa Kabwili tayari amelizungumza hili, watampa ushirikiano wote ili kukomesha matukio haya ya rushwa ambayo yanachafua taswira ya soka la Tanzania.

Aidha Bumbuli amesema tukio hili lifungue njia kwa wadau wenye ushahidi wa matukio mengine ya rushwa katika soka hapa nchini wajitokeze hadharani ili kukomesha matukio haya.

"Sisi kama Yanga tutakaa na Kabwili kuzungumza nae kwa undani, Kabwili ni Mchezaji wa Yanga hivyo tutampa ushirikiano wa kutosha katika hili baada ya kumsikiliza," amesema

"Ni kweli wachezaji hawaruhusiwi kuongea na vyombo vya habari lakini kwa kuwa imetokea na Kabwili ni mchezaji wetu hayo mambo ni ya ndani ya klabu, lakini kuhusu hizo tuhuma tutashirikiana nae kuona mambo kama haya yanakoma kama ni kweli yapo"


"Niwaombe wadau wenye ushahidi pia wajitokeze sio katika hili tu, hata vitendo vingine kama hivi ili tukomeshe mambo kama haya kwenye mpira wetu"

UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE