Breaking News

UGONJWA WA KISUKARI UNAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

UGONJWA wa Kisukari mwilini hutokana na vyakula pamoja na vinywaji tunavyotumia kila siku na hutumika kuupa mwili nguvu. Dk Godfrey Chale anafafanua maradhi haya:

Ugonjwa huu wa kisukari ni miongozi mwa sababu za ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume. Lakini unaweza ukajiuliza kuna uhusiano gani kati ya kisukari na upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume?

Tatifi mbalimbali za afya zinaonyesha kuwa asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.
Endapo kiwango cha sukari kwenye damu kikiwa juu kuliko kawaida huweza kusababisha madhara mengi sana mwilini, kama vile figo, moyo, shinikizo la damu, ulemavu wa viungo na upofu.
Pia, huathiri mfumo na miship ya fahamu, damu na hurudisha nyuma uchumi wa nchi kwa sababu huongeza watu wenye ulemavu na katika matibabu pia ni gharama kubwa. Kwa upande wa afya ya mfumo wa nguvu za kiume, lazima ubongo uwe imara na wenye afya, mishipa ya damu na fahamu iwe katika afya njema.

Kisukari hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo (Homoni) aina ya insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka kwa sukari (Hyperglycemia) au kushuka kwa kiwango cha sukari (Hypoglycemia). Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa na kuwa na kiwango kidogo cha insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili.

Watu wenye kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko inavyotakiwa kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu. Hii ni kutokana na moja ya sababu zifuatazo; huenda kongosho zao haziwezi kutengeneza insulini ya kutosha au seli za mwili wao haziathiriwi na insulin kama inavyotakiwa au sababu zote hizo mbili.

Kula sukari nyingi sio sababu ya ugonjwa wa kisukari. Lakini lazima tuseme kwamba kula sukari nyingi si nzuri kwa afya yako kwani utaongeza uzito wa kuweza kuathiri uwezo wa mwili wako kujikinga na maradhi tofauti.
Watu walio katika makundi yafuatayo wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kisukari: ni pamoja na wenye uzito uliozidi, wenye historia ya kuwa na wagonjwa wa kisukari katika familia zao, wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi, watu wasiojishughulisha au wasiofanya mazoez.
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati, kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani, kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri, kusikia njaa kila wakati na kula sana, wanawake kuwashwa ukeni. Kutoona vizuri, kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake au ganzi

DAWA
Kwa dawa za hospitali mpaka sasa hakuna dawa ya moja kwa moja ya kuponya lakini kwa aina ya pili ya ugonjwa, vyakula vinaweza kusawazisha hali hii kama ugonjwa haujakomaa. Wahi kupimwa hospitali.

MAKALA NA ELVAN STAMBULI

UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE