CHAMA AWASILI NA KUJIUNGA NA KAMBI YA SIMBA
Kiungo wa Kimataifa wa Zambia anayekipiga na mabingwa wa nchi, Simba Clatous Chama, amewasili nchini mchana wa leo Jumapili na kuungana na kikosi cha timu hiyo.
Mwamba huyo kutoka jiji la Lusaka anatarajiwa kuelekea kambini moja kwa moja na kuanza mazoezi baada ya kufanyiwa vipimo vya afya.
Sasa ni nyota mmoja tu wa kigeni wa Klabu hiyo ambaye bado hajarejea, Sharaff Abdulhaman Shiboub kutoka nchini Sudan.