Breaking News

KMC FC YAICHAPA YANGA MCHEZO WA KIRAFIKI

Kikosi cha Yanga leo kimeonja joto ya jiwe baada ya kuchapwa mabao 3-0 na KMC FC  Katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Vijana wa Yanga hawakuwa na mchezo mzuri hasa kwenye kipindi cha kwanza, wakiruhusu mabao mawili kupitia kwa Sadala Lipangwile dakika ya 31 na Charles Ilanfya dakika ya 45.

Kipindi cha pili kidogo vijana wa Mkwasa walizinduka lakini hata hivyo wakajikuta wanaruhusu bao la tatu lililofungwa na Hassan Kabunda kupitia mpira wa adhabu kwenye dakika ya 65.

Matokeo hayo ni ujumbe kwa benchi la ufundi pamoja na wachezaji kuwa wana kazi ngumu ya kufanya vizuri kwenye mechi zilizobaki kama mambo hayatabadilika.

Aidha benchi la undi lina wiki moja ya kusahihisha makosa kabla ya mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa June 13,2020 mkonani Shinyanga.