TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMAMOSI JUNE 06,2020
Klabu ya Manchester United imeweka kipaumbele katika usajili wa nahodha wa Aston Villa Jack Grealish, 24, msimu huu lakini inaweza kubadili mipango yake ikiwa mchezaji Kai Havertz wa klabu ya Bayer Leverkusen atapatikana. (Manchester Evening News)
Hata hivyo, Bayern Munich inaamini kwamba inakaribia kuzipiku klabu nyingine ikiwemo United katika usajili wa mchezaji huyo, United imekuwa ikiongoza kwa klabu zilivyoonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji Havertz 20, kati ya klabu nyngine maarufu za Ulaya. (Independent)
Manchester City imewasiliana na Barcelona kuhusu mshambuliaji Sergi Roberto. Lakini mchezaji huyo wa Uhispania 28, ataondoka Nou Camp ikiwa tu klabu hiyo itamuarifu kwamba sasa anaweza kuhamia kwingineko. (Mundo Deportivo, in Spanish)
Kiungo wa kati wa Newcastle United, Matty Longstaff 20, huenda akaishia katika mahasimu wao wa Ligi ya England Watford ikiwa atafikia makubaliano ya usajili.
Inter Milan inaweza kufikiria uwezekano wa kumuuza mshambuliaji wa Slovakia Milan Skriniar, ambaye amehusisha na Manchester City, ikiwa tu watapokea pendekezo la kumuuza mchezaji huyo kwa zaidi ya thamani ya €80m. (Tuttosport via Manchester Evening News)
Leicester City haina haraka ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Ben Chilwell, ikiamini kwamba kufuzu kwa msimu ujao katika Ligi ya Mabingwa kutawaweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kuwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Leicester Mercury)
Wakati huohuo, Leicester, maarufu kama The Foxes, wanataka angalau £60m kwa mchezaji Chilwell 23.(Guardian)
Winga wa Manchester City Leroy Sane atasaini mkataba wa miaka mitano na Bayern Munich. Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani 24, hatakuwa mchezaji mwenye kulipwa kiwango cha juu zaidi katika Ligi ya Ujerumani. (Bild)
Everton iko tayari kumtafuta nahodha wa Paris St-Germain Thiago Silva, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa Juni. Timu ya awali ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil 35, AC Milan pia imeonesha nia ya kutaka kumsajili. (Le10Sport)