TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMAPILI JUNE 07,2020
Klabu ya Real Madrid imewasilisha ombi la Euro 80 milioni (£71m) kumnunua kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Kai Havertz na itamruhusu mchezaji huyo kusalia katika klabu yake msimu ujao kabla ya kuelekea katika uwanja wa Bernabeu. (ESPN via Bild)
Manchester United imeimarisha hamu yake ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Ajax na Uholanzi Donny van de Beek, 23. (Sunday Times - subscription required)
Kiungo wa kati wa England na Aston Villa Jack Grealish 24, amempiku mchezaji mwenzake anayechezea Borussia Dortmund winger Jadon Sancho 20, kama mchezaji anayelengwa sana, na Manchester United mwisho wa msimu huu. (Sunday Mirror)
Manchester United huenda ikampatia winga wa Wales Daniel James 22, kandarasi mpya kabla ya kumuuza kwa mkopo msimu ujao. (Sun on Sunday)
Mchezaji anayelengwa na Manchester United na Chelsea Federico Chiesa ameambiwa anaweza kuondoka katika klabu ya Fiorentina. Mmiliki wa klabu hiyo anasema kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Italia anaweza kuondoka. (Football Italia)
Chelsea itasikiliza ofa za wachezaji kadhaa kutokana na kuwasili kwa winga wa Morocco na Ajax Hakim Ziyech 27, na mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner 24, kutoka klabu ya RB Leipzig mwisho wa msimu huu . (Daily Star Sunday)
Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Red Bull Leipzig Oliver Mintzlaff amekana kwamba Chelsea imefanikiwa kulipa £53m kama kifungo cha sheria cha kandarasi ya Werner akisema kwamba hakuna klabu iliyofanikiwa kutumia kandarasi ya uhamisho wowote. (Sky Sports Germany via Metro)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amewataja Havertz na Werner kama wachezaji wazuri lakini akasisitiza kwamba ujio wa virusi vya corona ndio uliozuia klabu yake kuwasaini.. (Sky Sports)
FC Barcelona imefungua kandarasi mpya na mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi ,32 na kipa wa Ujerumani Marc- Andre ter Stegen ,28 . (Mundo Deportivo - in Spanish)