Breaking News

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO ALHAMISI YA AUGUST 29-2019

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer yupo tayari kusubiri hadi msimu ujao w ajoto kushinikiza kiungo cha ushambilizi , huku mchezaji wa kiungo cha mbele wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19, akisalia kuwa mchezaji anayemlenga pakuu. (Evening Standard).
Barcelona na Paris St-Germain zimekubali malipo ya uhamisho wa mchezaji wa miaka 27 wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, lakini majadiliano yanaendelea kuhusu makubaliano ya mkataba huo. PSG inataka mchezaji wa kiungo cha mbele wa Ufaransa Ousmane Dembele, mwenye umri wa miaka 22, kuwa sehemu ya mpangilio huo. (Mirror)
Hatahivyo, Ajenti wa Dembele anasema mchezaji huyo hatoondoka Nou Camp, hatua ambayo huenda ikachangia kupromoka kwa pendekezo la uhamisho wa Neymar kwenda Barcelona. (Daily Mail).
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, mwenye umri wa miaka 25, amekubali makubaliano ya kujiunga upya na Monaco kwa mkopo – huku kukipangiwa malipo ya £31.8m ka mkataba wa kudumu.(RMC Sport, kupitia Sun)
Ousmane DembeleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mlinzi wa Arsenal Nacho Monreal, mwenye umri wa miaka 33, c huenda akarudi katika klabu alikotoka Uhispania kaba ya kufungwa dirisha la uhamisho Ulaya Jumatatu, huku Real Sociedad ikiwa na hamu kubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Osasuna na Malaga. (Evening Standard)
Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya England Sam Greenwood, mwenye umri wa miaka 17, ametambuliwa na timu bingwa ya Italia AC Milan na Juventus kama mchezaji anayelengwa baada ya kuridhisha maajenti katika mshindano ya ubingwa wa Ulaya wa timu za wachezaji walio chini ya umri wamiaka 17 mapema msimu huu wa joto. (Sun)
Manchester United italipa kitita cha £300,000 cha malipo ya Alexis Sanchez ya £400,000 kwa wiki wakatimchezaji huyo wa kiiungo cha mbele wa Chile akiwa uhamishoni kwa mkopo huko Inter Milan. (Metro)
Alexis Sanchez alijiunga na Manchester United mnamo Januari 2018Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlexis Sanchez alijiunga na Manchester United mnamo Januari 2018
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa RB Leipzig na anayelengwa na Liverpool, Timo Werner, mwenye umri wa miaka 23, bado hajakata tamaa ya uhamisho kwenda ng’ambo katika siku za usoni licha ya mchezaji huyo wa kiungo cha mbele wa timu ya taifa ya Ujerumani kusaini mktaba mpya katika klabu hiyo kwenye ligi ya Bundesliga. (Mirror)
Kipa wa Bournemouth Asmir Begovic, mwenye umri wa miaka 32, huenda akaondoka baada ya kuipoteza nafasi yake kwa mchezaji wamiaka 21 wa England Aaron Ramsdale. (Sun)
Mshambuliaji wa Reading Sam Baldock, mwenye umri wa miaka 30, anavutia vilabu kadhaa katika ligi ya Ujerumani Bundesliga 2, huku mlinzi mwenye miaka 19 wa timu ya taifa ya England Tom Holmes akitarajiwa kujiunga na KSV Roeselare huko Ubelgiji kwa mkopo. (Get Reading)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Stoke City Giannelli Imbula, mwenye miaka 26, anakaribia kuhamia kwa mkopo kwenda klabu katika ligi ya Serie A. (Sport Italia)

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.