Breaking News

DK: MSOLLA AWAITA MASHABIKI TAIFA


Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa, uwanja wa Taifa, Jumamosi hii.

Septemba 14 Klabu hiyo itashuka dimba hilo la Mkapa kuikabili Zesco United katika mchezo wa kwanza kusaka nafasi ya kutinga makundi.

Dk Msolla amesema ameridhishwa na maandalizi ya timu jijini Mwanza, ana matumaini makubwa kuelekea mchezo wa Jumamosi.

"Tunafanya maandalizi mazuri Mwanza, Mwalimu ameendelea kuwaweka vijana sawa kwa mchezo huo"

"Timu yetu iko vizuri, mashabiki waje kwa wingi Jumamosi waone Burudani," amesema

Aidha akizungumzia mwenendo wa timu hasa baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Pamba, Dk Msolla amesema kuna tofauti kati ya mechi ya mashindano na mechi ya kirafiki.

"Hii michezo ya kirafiki tunayocheza sio mashindano, ni sehemu ya mazoezi. Mwalimu anaitumia kujaribu mbinu na kurekebisha mapungufu yaliyopo"

"Lakini mechi za mashindano huwa tofauti"

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.