Breaking News

KINDOKI KUANZA KAZI KWENYE MECHI HII


Mjumbe wa Kamati ya Hamasa Jimmy Mshindo (aka Jimmy Kindoki) amesema baada ya uongozi wa Yanga kumpa nafasi hiyo, kazi yake anaianza rasmi kuelekea mchezo dhidi ya ZESCO United.

Kindoki ni miongoni mwa wajumbe walioteuliwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga kuunda Kamati ya Hamasa.

"Naushukuru uongozi huu mpya wa Yanga unaongozwa na Dr Msolla pamoja na Makamu wake Mwakalebela, wajumbe wote, matawi na wanachama kwa kunipa nafasi hii"

"Mungu aniongoze ili nioneshe kipaji changu. Hakika sasa Yanga imezaliwa upyaaaaaaaaa"

Kabla ya uteuzi huo Kindoki alifahamika zaidi kwa kujitoa kwake katika masuala mbalimbali yanayoihusu klabu ya Yanga.

Wanayanga wengi walimpigia 'chapuo' kupewa kitengo cha uhamasishaji katika klabu ya Yanga.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.