Achomwa kisu shingoni baada ya kummwagia mwenzie maji machafu siku ya 'birthday
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma amethibitisha tukio la Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Ufundi Trade Peramiho wilayani Songea, Grayson Maselin (23), kumjeruhiwa mwanafunzi mwenzake Mosses Ngole (23), kwa kuchomwa kisu shingoni baada ya kummwagia maji machafu siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake (birthday).
Alidai kuwa, siku ya tukio, Ngole alikuwa analazimishwa kumwagiwa maji na kupakwa matope na wanafunzi wenzake ndipo alipopandisha hasira na kufikia uamuzi wa kumchoma kisu mwanafunzi mwenzake huyo.
Kamanda Maigwa alidai mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi mwenzake, ambaye kwa sasa amelazwa Hospitali ya Kanisa Peramiho.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE