Breaking News

BONDIA HASSAN MWAKINYO KAMPIGA ARNEL TINAMPAY KWA POINT

Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo amefanikiwa kushinda pambano kati yake na Mfilipino, Arnel Tinampay lililofanyika usiku huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo la uzito wa Super Welterweight limemalizika huku majaji wawili wakimpa ushindi Mwakinyo wa 97-93 na 98-92 huku jaji mmoja akitoa sare ya 96-96.
Akizungumza baada ya pambano hilo, Mwakinyo ameeleza kuwa lilikuwa pambano gumu zaidi kwake na kwamba amejifunza mengi kutoka kwa bondia huyo mzoefu ambaye hajawahi kupigwa ‘KO’.
“Wakati ninawaeleza watanzania kuwa ninaenda kupambana na bondia Mfilipino niliwaambia ni bondia mgumu sana, lakini leo nimejifunza kitu kingine kutoka kwake, ni bondia mvumilivu sana na alikuwa akinichezea kwa karibu sana.
Akizungumza kwenye ulingo baada ya pambano hilo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alimpongeza Mwakinyo kwa kazi nzuri aliyoifanya akieleza kuwa amevunja rekodi tangu tupate uhuru kwa kuujaza uwanja wa Uhuru kupitia masumbwi.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE