Breaking News

MKWE WA FRAGA AIBUA MASWALI MSIMBAZI


Kwa wasiomfahamu wakala wa kiungo mkabaji wa Simba Gerson Fraga ni mkwe wake kabisa, ambaye yuko nchini kuangalia maendeleo ya mteja wake.

Juzi kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting 'mkwe' huyo alipata nafasi ya kupanda basi la klabu ya Simba kuingia uwanjani kushuhudia mtanange huo uliopigwa uwanja wa Uhuru na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Kutokana na tetesi zinazoendelea kuhusu kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems, wapo waliodhani Baba mzaa chema huyo wa Fraga yuko kwenye mazungumzo ya kuinoa Simba kwani hata alipokuwa uwanjani akishuhudia mchezo, alikuwa akionekana kuandika mambo mbalimbali kwenye notibuku yake.

Picha zake zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kukifanyika upotoshaji wa kuwaaminisha Wanamsimbazi kuwa uyo ndiye mrithi wa Aussems.

Mwenyewe ameshangazwa na kusambazwa kwa picha hizo huku akisisitiza hana taaluma ya ukocha.


"Mimi si kocha, bali napenda soka nilichokuwa naandika kama ulikuwa unanifuatilia kinamuhusu Gerson Fraga, ni Mkwe wangu," alisema
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE