Breaking News

VIDEO: TAMASHA LA ALIKIBA MWANZA LAAHIRISHWA, YEYE ATOA SABABU HIZI

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ali Salehe Kiba alimaarufu Ali Kiba amefunguka kuhusu tamasha lake la Alikiba Uniforgetable kuahiriswa mkoani Mwanza sehemu ambako lilikuwa linaenda kuzinduliwa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika haya:-
“Kutokana na masuala mbalimbali ya kiserikali yanayoendelea jijini Mwanza kutoka sasa mpaka kilele cha siku ya Uhuru wa Tanzania, imepelekea kufikia maamuzi ya kusogeza mbele matukio ya UNFORGETTABLE TOUR MWANZA mpaka nitakapowatangazia tarehe mpya ndani ya mwezi ujao. Hivyo nimeamua rasmi kwamba #AlikibaUnforgettableTour tunaenda kuizundulia mkoani Tabora aka TORONTO.
Shughuli zinaanza rasmi kuanzia Jumatano hii mpaka Jumamosi ya tarehe 30 katika dimba la Ali Hassan Mwinyi. Kwa Kiingilio cha 10,000 utashuhudia mambo makubwa kwa mara ya kwanza tangu nimeanza muziki. Taarifa zaidi zitakujia.”

Lakini baada ya Tamasha hilo kuahirishwa Mwanza sasa limehamia Tabora:-

UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE