Breaking News

VIDEO: UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, CCM YASHINDA KWA ASILIMIA 99.9

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo aliyatangaza matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo CCM imeshinda Vijiji 12,260 (99.9%), Mitaa 4262 (100%), Vitongoji 63,970 (99.4%) ambayo inatajwa ni sawa na asilimia 99.9.

Amesema kuwa, pia chama hicho kimeshinda katika Mitaa 4,263 sawa na asilimia 100, huku kikishinda Vitongoji 63,970 sawa na asilimia 99.4.
Amebainisha kuwa, CHADEMA kimeshinda nafasi moja ya Wenyeviti wa Vijiji, hakikufanikiwa kupata Mtaa, Wenyeviti wa Vitongoji kimepata nafasi 19, Wajumbe kundi la Wanawake imepata nafasi 39 na Wajumbe kundi mchanganyiko imepata nafasi 7. Chama cha CUF kimepata nafasi moja ya Kijiji, Mitaa miwili, Wajumbe Kundi la Wanawake wamepata nafasi tatu, na Wajumbe kundi mchanganyiko wamepata nafasi 14.

Chama cha ACT Wazalendo, hakikufanikiwa kupata Mwenyekiti wa Kijiji, hakikufanikiwa kupata Mtaa, lakini imefanikiwa kupata Mwenyekiti wa Kitongoji mmoja, Mjumbe moja wa kundi la wanawake na wajumbe 11 wa kundi mchanganyiko.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE